32. Nao ndugu zao wengine wa ukoo wa Kohathi walikuwa na wajibu wa kutayarisha mikate ya wonyesho kwa ajili ya hekalu kila Sabato.
33. Jamaa nyingine za Walawi zilisimamia huduma ya nyimbo hekaluni. Waliishi katika baadhi ya majengo ya nyumba ya Mungu na hawakuhitajika kufanya kazi nyingine yoyote kwa maana walikuwa kazini usiku na mchana.
34. Watu wote hawa waliotajwa walikuwa viongozi wa kabila la Walawi, kulingana na koo zao. Wao ndio viongozi walioishi Yerusalemu.