1 Mambo Ya Nyakati 6:12-17 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Ahitubu alimzaa Sadoki, Sadoki alimzaa Meshulamu,

13. Meshulamu alimzaa Hilkia, Hilkia alimzaa Azaria,

14. Azaria alimzaa Seraya, Seraya alimzaa Yehosadaki;

15. Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza.

16. Lawi alikuwa na wana watatu: Gershomu, Kohathi na Merari.

17. Kila mmoja wao pia alikuwa na wana. Gershomu aliwazaa Libni na Shimei;

1 Mambo Ya Nyakati 6