1 Mambo Ya Nyakati 5:2-6 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Ingawa kabila la Yuda ndilo lililokuja kuwa lenye nguvu zaidi kuliko mengine, na watawala walitoka humo, haki ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yosefu).

3. Wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa Henoki, Palu, Hesroni na Karmi.

4. Wazawa wa Yoeli toka kizazi hadi kizazi walikuwa Shemaya, Gogi, Shimei,

5. Mika, Reaya, Baali,

6. na Beera, ambaye mfalme Tiglath-pileseri wa Ashuru, alimchukua mateka ingawa alikuwa kiongozi wa Wareubeni, akampeleka uhamishoni.

1 Mambo Ya Nyakati 5