1. Wana wa Yuda walikuwa Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.
2. Reaya, mwana wa Shobali, alimzaa Yahathi, aliyekuwa baba yake Ahumai na Lahadi, hizo ndizo jamaa za Wasorathi.
3. Wana wa Etamu walikuwa Yezreeli, Ishma na Idbashi. Walikuwa na dada mmoja aliyeitwa Haselelponi.
4. Penueli aliwazaa Gedori na Ezeri, na Ezeri akamzaa Husha. Hao ndio wazawa wa Huri mzaliwa wa kwanza wa Efratha, baba yake Bethlehemu.
5. Ashuru, mwanzilishi wa mji wa Tekoa, alikuwa na wake wawili: Hela na Naara.
6. Naara alimzalia wana wanne: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.
7. Hela alimzalia wana watatu: Serethi, Ishari na Ethnani.