1 Mambo Ya Nyakati 2:34-40 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Sheshani hakuwa na watoto wa kiume; alikuwa na binti tu. Hata hivyo, alikuwa na mtumwa wa Kimisri, jina lake Yarha.

35. Hivyo, Sheshani akamwoza Yarha mtumwa wake, mmoja wa binti zake, naye akamzalia mwana jina lake Atai.

36. Atai alimzaa Nathani, Nathani akamzaa Zabadi.

37. Zabadi akamzaa Eflali, Eflali akamzaa Obedi,

38. Obedi akamzaa Yehu, Yehu akamzaa Azaria,

39. Azaria akamzaa Helesi, Helesi akamzaa Eleasa,

40. Eleasa akamzaa Sismai, Sismai akamzaa Shalumu,

1 Mambo Ya Nyakati 2