1 Mambo Ya Nyakati 2:32-35 Biblia Habari Njema (BHN)

32. Yada, nduguye Shamai, alikuwa na wana wawili: Yetheri na Yonathani. Lakini Yetheri alifariki bila watoto.

33. Yonathani alikuwa na wana wawili: Pelethi na Zaza. Wote hao ni wazawa wa Yerameeli.

34. Sheshani hakuwa na watoto wa kiume; alikuwa na binti tu. Hata hivyo, alikuwa na mtumwa wa Kimisri, jina lake Yarha.

35. Hivyo, Sheshani akamwoza Yarha mtumwa wake, mmoja wa binti zake, naye akamzalia mwana jina lake Atai.

1 Mambo Ya Nyakati 2