1 Mambo Ya Nyakati 2:25-32 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, alikuwa na wana watano: Ramu, mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.

26. Yerameeli alikuwa na mke mwingine jina lake Atara. Huyu alimzalia Yerameeli mwana, jina lake Onamu.

27. Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini na Ekeri.

28. Wana wa Onamu walikuwa Shamai na Yada. Nao wana wa Shamai walikuwa Nadabu na Abishuri.

29. Abishuri alioa mke, jina lake Abihaili, naye akamzalia wana wawili: Abani na Molidi.

30. Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu; lakini Seledi alifariki bila watoto.

31. Apaimu alikuwa na mwana mmoja aliyeitwa Ishi. Ishi alimzaa Sheshani, na Sheshani akamzaa Alai.

32. Yada, nduguye Shamai, alikuwa na wana wawili: Yetheri na Yonathani. Lakini Yetheri alifariki bila watoto.

1 Mambo Ya Nyakati 2