1 Mambo Ya Nyakati 2:18-22 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Kalebu, mwana wa Hesroni, kutokana na wake zake wawili, Azuba na Yeriothi, aliwazaa Yesheri, Shaobabu na Ardoni.

19. Azuba alipofariki, Kalebu alimwoa Efratha aliyemzalia Huri.

20. Huri alimzaa Uri, naye Uri akamzaa Besaleli.

21. Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, dada yake Gileadi. Huyo alimzalia mwana jina lake Segubu.

22. Segubu alimzaa Yairi ambaye alitawala miji mikubwa ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.

1 Mambo Ya Nyakati 2