1 Mambo Ya Nyakati 2:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Israeli alikuwa na wana wa kiume kumi na wawili: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuluni,

2. Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.

3. Wana wa Yuda waliozaliwa na Bethshua, mkewe Mkanaani, walikuwa Eri, Onani na Shela. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, basi Mwenyezi-Mungu akamuua.

4. Na Tamari, mkwewe, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Jumla, wana wa Yuda walikuwa watano.

5. Peresi alikuwa na wana wawili: Hesroni na Hamuli.

1 Mambo Ya Nyakati 2