1 Mambo Ya Nyakati 16:28-35 Biblia Habari Njema (BHN)

28. Mpeni Mwenyezi-Mungu, heshima enyi jamii zote za watu,naam, kirini utukufu na nguvu yake.

29. Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima ya utukufu wa jina lake;leteni tambiko na kuingia nyumbani mwake.Mwabuduni Mwenyezi-Mungu patakatifuni pake.

30. Ee dunia yote; tetemeka mbele yake!Ameuweka ulimwengu imara, hautatikisika.

31. Furahini enyi mbingu na dunia!Yaambieni mataifa, “Mwenyezi-Mungu anatawala!”

32. Bahari na ivume, pamoja na vyote vilivyomo!Furahini enyi mashamba na vyote vilivyomo!

33. Ndipo miti yote msituni itaimba kwa furahambele ya Mwenyezi-Mungu anayekujanaam, anayekuja kuihukumu dunia.

34. Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema,kwa maana fadhili zake zadumu milele!

35. Mwambieni Mwenyezi-Mungu:Utuokoe, ee Mungu wa wokovu wetu,utukusanye pamoja na kutuokoa kutoka kwa mataifa,tupate kulisifu jina lako takatifu,kuona fahari juu ya sifa zako.

1 Mambo Ya Nyakati 16