19. Idadi yenu ilikuwa ndogo,mlikuwa wachache na wageni katika nchi ya Kanaani,
20. mkitangatanga toka taifa hadi taifa,kutoka nchi moja hadi nchi nyingine,
21. Mungu hakumruhusu mtu yeyote awadhulumu;kwa ajili yao aliwaonya wafalme:
22. “Msiwaguse wateule wangu;msiwadhuru manabii wangu!”
23. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu, ulimwengu wote.Tangazeni kila siku matendo yake ya wokovu.
24. Yatangazieni mataifa utukufu wake,waambieni watu wote matendo yake ya ajabu.
25. Maana Mwenyezi-Mungu ni mkuu, anasifika sanaanastahili kuheshimiwa kuliko miungu yote.
26. Miungu yote ya mataifa mengine si kitu;lakini Mwenyezi-Mungu aliziumba mbingu.
27. Utukufu na fahari vyamzunguka,nguvu na furaha vyajaza hekalu lake.
28. Mpeni Mwenyezi-Mungu, heshima enyi jamii zote za watu,naam, kirini utukufu na nguvu yake.
29. Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima ya utukufu wa jina lake;leteni tambiko na kuingia nyumbani mwake.Mwabuduni Mwenyezi-Mungu patakatifuni pake.