26. Wanajeshi mashujaa wa Daudi walikuwa: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethlehemu,
27. Shamothi Mharodi, Helesi Mpeloni,
28. Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa, Abiezeri Mwanathothi;
29. Sibekai Mhushathi; Ilai Mwahohi;
30. Maharai Mnetofathi; Heledi, mwana wa Baana Mnetofathi;
31. Itai, mwana wa Ribai, kutoka Gibea, wa kabila la Benyamini; Benaya Mpirathoni;
32. Hurai kutoka vijito vya Gaashi, Abieli Mwaibathi;
33. Azmawethi Mbaharumu; Eliaba Mshaalboni;