28. Abrahamu alikuwa na watoto wawili wa kiume: Isaka na Ishmaeli.
29. Hivi ndivyo vizazi vyao: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli alikuwa Nebayothi na wengine ni Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
30. Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
31. Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32. Abrahamu alikuwa na suria aliyeitwa Ketura. Ketura alimzalia Abrahamu: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
33. Wana wa Midiani walikuwa: Efa, Eferi, Henoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wazawa wa Ketura.
34. Isaka, mwana wa Abrahamu, alikuwa na wana wawili: Esau na Israeli.
35. Wana wa Esau walikuwa Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
36. Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna na Amaleki.
37. Wana wa Reueli walikuwa Nahathi, Zera, Shama na Miza.